- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ACT WAZALENDO YAAHIDI KUFUTA KESI ZA KISIASA NCHINI
Sambamba na hilo amesema pia watazifuta kesi za watu waliobambikiziwa na kuwalipa fidia waliolipishwa fedha mahakamani.
Ahadi hiyo ameitoa leo Jumamosi Machi 14, 2020 katika mkutano wa pili wa mwaka wa chama hicho unaofanyika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam unaokwenda sambamba na uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema katika kipindi cha miaka minne iliyopita watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa vyama vya upinzani na wafanyabiashara wamekuwa wakibambikiwa kesi bila ya kuwa na makosa yoyote huku wengine wakilipishwa fedha.
“Kwanza tutapambana na rushwa na kuondoa vikwazo walivyowekewa watu wote walioonewa katika kipindi cha miaka minne kwa kubambikiwa kesi ili kuhakikisha kwanza wanaachiwa huru.”
“Kwa wale waliohukumiwa adhabu mbalimbali kwa uonevu watafutiwa rekodi za adhabu zao na kurudishiwa fedha walizotozwa kwa sababu hiyo ni ndoto ya ACT- Wazalendo,” amesema
Kwa upande wa wafanyabiashara, amesema wamelenga kuwawekea mazingira mazuri ya ufanyaji biashara halali lakini pia kuhakikisha mnalipa kodi zenu na kutonyonya wafanyakazi wenu.
Amesema kufanya hivyo kutawapa motisha ya kuzalisha zaidi ili kuongeza ajira na kupanua pato la taifa.
“Nasema hivyo kwa sababu katika kipindi cha miaka mitano ya CCM imewaacha hiloi kwa kuwabambikia makodi makubwa na kuwafunga jela na wengi wenu kukimbia nchi,” amesema Zitto