- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: ACACIA YAKUBALI KUILIPA TANZANIA KWA MASHARTI
Dar es salaam: Kampuni ya madini ya ACACIA imesema kuwa ipo tayari kulipa tozo mpya ya madini ya mrabaa kati ya asilimia 4 mpaka 6, lakini pamoja na kukubali huko ACACIA Imesema kuwa inaendelea kufanya tathimini ya sheria mpya ya madini iliyo pitishwa siku za hivi karibuni na bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania tangu kutokea kwa kashfa ya makinikia,
ambapo serekali ya Tanzania ilishutumu kampuni ya Acacia kwa kuendesha biashara yake bila kutoa taarifa sahihi juu ya kiwango halisi cha madini yaliyomo kwenye mchanga.
Mwezi machi mwaka huu Rais Magufuli alizuia usafirishaji wa makontena ya mchanga wa dhahabu 256 kwenye bandari ya Dar es salaam, ambapo Acacia walilaani hatua hiyo kwa kile wanachoamini kuwa Rais magufuli hapewi taarifa sahihi na watendaji wake kwa upande wa madini.