Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:47 am

NEWS: ABIRIA WALIOKWAMA AFRIKA KUSINI WATAFUTIWA USAFIRI MBADALA

Dar es Salaam. Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Ladislaus Matindi amesema abiria wa ndege ya Air Tanzania iliyozuiwa kuondoka katika uwanja wa ndege wa Oliver Tambo, Johannesburg nchini Afrika Kusini Iwametafutiwa usafiri mbadala.

Image result for abiria wa airtanzania

Mtindi ameliambia gazeti la Mwananchi Jumamosi ya leo Agosti 24, 2019 kuwa abiria wote waliokuwa katika ndege hiyo wametafutiwa usafiri mwingine, wapo walioanza kuwasili jijini Dar es Salaam.

“Tutahakikisha abiria wote waliokata tiketi wanasafiri kama ilivyopangwa, huwa kuna makubaliano katika mashirika ya ndege kwamba unapopata tatizo kama hili nani anakusaidia.” amesema Mtindi

“Suala la kupeleka ndege nyingine kwa safari ya Afrika kusini itategemea ni jambo la kusubiri suala lenyewe kwanza liwe wazi kujua kwa nini kimetokea na nini kinafuata. Hili ni suala la kisheria hivyo itatokana na namna litakavyokuwa limetatuliwa lakini sisi tutaendelea kuihudumia hiyo njia.”

Taarifa ya kuzuiliwa kwa ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Afrika Kusini kwenda Dar es Salaam, Tanzania ilitolewa jana Ijumaa Agosti 24, 2019 na katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Leonard Chamuriho.

Alibainisha kuwa inashikiliwa kwa amri ya mahakama kuu ya Gauteng, Johannesburg na Serikali inafuatilia suala hilo ili iweze kuachiwa mara moja.

Matindi amesema kuna safari zitaathirika kutokana na kushikiliwa kwa ndege hiyo moja aina ya Airbus A220-300 na abiria ambao tayari wamekata tiketi wataarifiwa iwapo katika safari husika kutakuwa na mabadiliko yoyote au ipo kama ilivyopangwa.

Leo asubuhi shirika hilo la ndege kupitia mtandao wake wa twitter umetanganza kufanya mabadiliko ya safari zake za ndege kutokana na kadhia hiyo

"Wapendwa Wateja Wetu, kutokana na sababu zilizopo nje ya uwezo wetu, Air Tanzania inasikitika kuwataarifu kuwa kutakuwa na mbadiliko ya ratiba za ndege.

"Tuna waomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza kwenye ratiba/mipango ya safari zenu." imeseama sehemu ya ujumbe wake.