- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: 39 WANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPIGWA NA RADI
Geita. Wanafunzi 39 wa darasa la nne Shule ya Msingi Ihumilo Mkoani Geita wamenusurika kifo baada ya kupigwa na radi wakati wakiwa darasani.
Kwa mujibu wa Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Oktoba 18, 2019 na mganga mkuu wa mkoa huo, Josephat Simeo inasema kuwa wanafunzi 24 wamepelekwa katika hospitali ya wilaya ya Nzera na 15 wamepatiwa matibabu katika zahanati ya Nkome baada ya Ajali hiyo.
Dk Simeo ameeleza kuwa radi hiyo imesababisha watoto kupata mshtuko na kuzimia lakini baada ya kupatiwa huduma ya kwanza wanaendelea vizuri na tayari wanafunzi 36 wameruhusiwa kutoka hospitali.
Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Kaitila Murusuri amesema aliwapokea wanafunzi 24 saa 2 asubuhi kwamba walikuwa wamepata mshtuko, waliwapatia huduma ya kwanza.
β21 kati yao wameruhusiwa kutoka hospitali, watatu ambao hali zao si nzuri wanaendelea na matibabu,β amesema.