- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: 23% YA WASICHANA KUKATISA UTOTO WAO KUTOKANA NA NDOA ZA UTOTONI
DODOMA : IMEELEZWA kuwa asilimia 23 ya wasichana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 19 hapa nchini hukatishwa utoto wao kutokana na ndoa za utotoni ambapo mimba za utotoni yani kiwango cha kuzaa kwa wasichana ni watoto asilimia 117.7 kwa kila watoto1000.
Takwimu hizo zimetolewa leo Mjini Dodoma katika Kongamano la maadhimisho ya mtoto wa Afrika na Mshauri wa haki za watoto na utawala bora wa Shirika la Save the Children,NEEMA BWAIRA wakati akitoa taarifa ya ripoti hiyo ya kidunia inayoitwa nafasi ya mwisho wa utoto ambayo imefanyika katika nchi 172 Duniani ambayo ina viashiria nane.
Kufuatia kuwepo kwa viashiria hivyo Mshauri huyo ametoa mapendekezo mbalimbali ambayo ripoti hiyo inajielekeza.
Hata hivyo amewataka wadau mbalimbali kwakushirikiana na Serikali kuwekeza kwa watoto ikiwa ni pamoja na kutoa huduma sawa kwa watotona kuondokana na mila potofu za ubaguzi wa kisera na kimilaa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia ,wazee na watoto,DKT.HAMISI KIGWANGALA ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo,amesema kuwakatika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imetenga zaidi ya ShilingiSh.Bilioni 15 kwaajili ya kutekeleza mpango wa huduma za ulinzi kwa watoto na wanawake.
Hata hivyo amesema kuwa suala la malezi kwa wazazi halipewi kipaumbele hususani kwa wazazi waishiomjini na hivyo kuathiri makuzi ya watoto.