Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:41 pm

NEWS: 17 MBARONI MKOANI DOM

DODOMA: JESHI la polisi mkoani Dodoma limekamatawatu 17 miongoni mwa hao watano [5] ni raia wa China .

Wakati wachina wakituhumiwa kukamtwa na nyara za serikali , waliosalia wanatuhumiwa kwa kuvunja na kuiba.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Gilles Muroto amesema watuhumiwa hao walikamatwa mnamo tarehe 11 mwezi wa 9 mwaka huu

Muroto amesema raia wa wachina walikamatwa katika kiwanda cha Sand industries Company Limited kilichopo kijiji cha Mpamatwa wilaya ya Bahi mkoani hapa kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali kinyume na sheria.

‘’ watuhumiwa hao walikamatwa na yara za serikali ambazo ni Magamba 652 ya mnyama kakakuona [pangolin], kucha tano [5] za kakakuona , kucha nne [4] za simba na jino moja [1] la simba ‘’ amesema Muroto.

Akifafanua kamanda Muroto amesema walikamata televisheniflat screen 13, printer ya computer 1, redio sabwoofer 2 , kiny’amuzi1, speaker5, buster ya gari 1 ,deck 1 na bhangi kete 12.

Amesema kati ya watuhumiwa waliokamatwa moja wao aaitwaye kwa jina Dotto Kapenga mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa chang’ombe alikamatwa akiwa na sare za jeshi la wananchi [JWTZ]aina ya kombati suruali , sweta mbili , mikanda mitatu , kofia tano, buti pea moja , koti la mvua na cheo cha luten ussu.

Kamanda Muroto ametoa Wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ilikukomesha uharifu katika mkoa wa Dodoma .

‘’wananchi endeleeni kutoa taarifa za wahalifu na uharifu kwa jeshi la polisi nasi tutazifanyia kazi kwa ukamilifu’’ amesema Muroto.