Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 8:50 am

NEW: MAKAMU WA RAIS AMEWAONYA WAKANDARASI KUACHA TABIA YAKUONGEZA GHARAMA ZISIZOKUWA NA TIJA.

Dodoma: Makamu wa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan amewataka makandarasi nchini kuacha tabia yakuongeza gharama ambazo haziendani na miradi mbalimbali ambayo wamekuwa wakipewa na Serikali.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani ametoa kauli hiyo mjini Dodoma katika mkutanao wa mashauriano wa Bodi ya usajili wa Makandarasi kwa mwaka kuweka msisitizo kwa makandarasi kufanya kazi kwa weledi.

Kwa upande wake mwakilishi wa Makandarasi Pastory Masota akazungumzia changamotohizo kuwa ni miradi mingi ya serikali inatolewa kinyume na tarabu za ujenzi ambapo huwa wanazifanya za manunuzi nahiyo inapelekea kuonekana hawana maana katika nchi hii.

Waziri wa Ujenzi,uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa amewatoa hofu baadhi ya wakandarasi juu ya madeni wanayoidai serikali Na kusema kuwa waiamini serikali ipo nainafanya kazi kwa ufanisi zaidi.