- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEW: CHINA YAJIBU TUHUMA ZA WAAFRIKA KUBAGULIWA NCHINI HUMO
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Uchina Zhao Lijian amesema Serikali ya Uchina inawachukulia wageni wote Nchini humo kwa usawa.
Kauli ya Kiongozi huyo inakuja Baada ya Waafrika wanaoishi nchini Uchina kulalamika kuwa wanabaguliwa na kufurushwa kwenye nyumba na hoteli, baada ya kutuma video na picha zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii za watu wanaodaiwa kuwa ni Waafrika waliokwama kwenye mitaa ya Uchina baada kufurushwa kwenye nyumba na hoteli na kubaki bila makazi.
Amesema Nchini Uchina kazi yetu ya dhahurura ni kuchukua hatua za kudhibiti mlipuko, amesema Lijian.
Tunafuatilia kwa hali ya juu matukio na kutolelewa kuliko jitokeza katka mchakato huu. Tunaomba mamlaka husika kuboresha kazi zake, tunatumai wote Wachina na Wageni nchini Uchina wanazingatia sheria za kukabiliana na janga, shirikiana na tuunge mkono katika mapambano dhidi ya virusi imesema taarifa ya ya twitter kupitia Ubalozi wa China nchini Kenya.
Baadhi ya Wakenya walioko nchini Uchina kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari nchini Kenya wamekua wakizungumzia masaibu wanayoyapitia baada ya kufurushwa na kubaguliwa huku wakinyimwa huduma kwa kile wanachodai wanaangaliwa kama wageni wanaosambaza virusi vya corona.
Wamekua wakiiomba serikali yao kurudi nyumbani kutokana na ubaguzi wa rangi dhidi ya Waafrika wanaoishi Uchina baada ya janga la virusi vya corona.
Taarifa za mateso wanayodaiwa kupitia Wakenya nchini Uchina zimeibua hisia kali hususan katika mitandao ya kijamii ambapo baadhi ya Wakenya wameomba uhusiano baina ya mataifa hayo mawili uchunguzwe upya.
Kupitia kampeni #ChinaMustExplain au #ChinaLazimaEeleze kwenye mitandao ya kijamii Wakenya wamekua wakielezea hisia zao kuhusu hali ya wenzao nchini Uchina, huku wengi wakiitaka serikali ya Kenya kuchukua hatua kunusuru raia hao.
Mbunge wa zamani wa Kiambuu William Kabogo kwenye ukurasa wake wa Twitter amemsihi rais Kenyatta Kutuma ndege kuwachukua Wakenya wanaoishi Uchina: