- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEW: BASHE NA SIMBACHAWENE WAAPISHWA LEO IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amewaapisha Waziri wa ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano George Simbachawene Na Naibu Waziri Kilimo Hussein Bashe katika hafla iliyofanyika leo Jumatatu Julai 22, 2019 ikulu Jijini Dare es salaam.
Simbachawene aliyejiuzulu Nafasi yake Kama Waziri wa TAMISEMI amechukua nafasi ya January Makamba aliyefutwa kazi mwishoni mwa juma hili
Simbachawene alijiuzulu wadhifa wake mara baada ya Ripoti ya Uchunguzi wa Madini ya Tanzanite kumtaja kuhusika katika sakata la Ubadhirifu.
“Kwanza kabisa Mhe. Rais napenda nichukue nafasi kukushukuru kwa dhati kabisa kuniamini tena kwa kunipa nafasi ya kukusaidia kama wa Waziri wa Nchi katika ofisi ya Makamu wa Rais nayeshugulikia Muungano na Mazingira”- amesema Simbachawene baada ya kuapishwa leo.
Naye kwa Upande wa Bashe alijikita katika kuelezea mkakati wa kuinua sekta ya kilimo mara baada ya kuapishwa
"Sekta ya kilimo tumekuwa tunaita tu kilimo cha kujikimu, ila nafahamu kilimo ni biashara na kilimo ni maisha
Nafahamu uchumi wa nchi hii ambapo ndoto yako ni kujenga uchumi wa viwanda ni lazima wakulima wawe na uwezo, tuwatendee haki" amesema Bashe