Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 3:40 pm

MWANASIASA WA UPINZANI CONGO AITAKA ICC KUMLIPA ZAIDI YA BILIONI 150

Mwanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jean-Pierre Bemba anaitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kumlipa zaidi ya euro milioni 68 sawa na Tsh. Bilioni 170 kama fidia kutokana na kumfunga bila hatia.

Image result for Jean-Pierre Bemba ICC

Kama utakumbuka mwanasiasa huyo alishtumiwa na mahakama hiyo kwa uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliotekelezwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati mwaka 2002 na 2003, lakini aliachiliwa huru mwezi Juni mwaka jana, baada ya kumaliza miaka kumi jela.

Baada ya kukamatwa kwake, Mahakama hiyo ilikamata mali zake, ikiwa ni pamoja na zile za nchini Ureno, Ubelgiji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Anaishtumu Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kumnyang'anya mali zake na hivyo kulipwa fidia.

Related image

Jean-Pierre Bemba anaomba fidia ya euro milioni 26 kwa miaka yote hiyo alikuwa gerezani akisema alifanyiwa unyonge kutokana na kutafsiri sheria vibaya, madai ambayo ofisi ya mashitaka ya ICC inapinga.

Lakini kwa fedha hizo, kuna euro milioni 42, ambazo anasema ni fidia kutokana na uharibifu wa mali zake.

Wakati wa kukamatwa kwake, ICC iliomba nchi kadhaa kuzuia mali zake: nyumba ya kifahari na ndege aina ya Boeing 737 huko Faro nchini Portugal, akaunti za benki ikiwa ni pamoja na baadhi ya ndege na ndege sita nchini DRC za shirika lake la ndege.