Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 12:21 am

MUSIC: HARMONIZE AOMBA KADI NYEKUNDU WCB, AVUNJA UTARATIBU WASAFI FESTIVAL

Msanii wa Bongo fleva kutoka nchini Tanzania kwenye Ardhi ya Nyerere Harmonize ameomba kuondoka kwenye label ya wasafi classic baby (WCB).

Kwamujibu wa Taarifa iliyotolewa jana Agosti 22, 2019 na Meneja mkuu wa label hiyo, Sallam SK maarufu kama Mendezi amesema kuwa Harmonize amomba zaidi ya mara kadhaa kujitoa WCB kwa kutaka kuvunja mkataba huku akiongezea kuwa kinachomfanya mpaka sasa msanii huyo kuendelea kuwepo kwenye label hiyo maarufu Afrika ni vipengele vya mkataba vinavyombana msanii huyo lakini kimoyo hayupo tena WCB.

Image result for diamond platnumz na harmonize

"Harmonize kwasasa hivi ndani ya moyo wake hayupo WCB, Kwanini nasema hivyo? Harmonize tayari ameshatuma maombi ya ku-terminate mkataba wake na WCB, Yupo tu kusubiri kupitia vifungu vyote vya mkataba ili kuvunja mkataba" amesema Sallam kwenye mahojiano yake na kituo cha radio cha Wasafi FM.

“Sisi tumependezwa na hatua yake kwa sababu labda kuna vitu ameona akivifanya atafika mbali,” amesema Sallam.

Aidha Sallam amezungumzia sababu za msanii Harmonize kutoonekani katika matamasha ya Wasafi Festival yanayoendelea mikoa mbalimbali nchini kwa kuwa amevunja utaratibu wa tamasha hilo kwa kujitenga na wenzake.

Image result for diamond platnumz na harmonize

Kuhusu kujitenga na wenzake Sallam amesema, “Hili jambo si sawa kulingana na maudhui ya tamasha hilo. Maudhui ya Wasafi Festival ni umoja. Msanii akiamua kuacha kuambatana na wasanii wenzake ambao wapo pamoja katika tamasha ni kwenda kinyume.

“Sisi katika tamasha letu hatupendi kutengeneza matabaka, tumeamua kuwa kitu kimoja, siyo kwamba Diamond, Rayvany hawakuwa na uwezo wa kutumia usafiri wao binafsi kama alivyofanya Harmonize” amesema Sallam.

Image result for sallam sk

Meneja huyo amewaomba radhi wasanii wote walioshiriki tamasha la Mwanza kutokana na Harmonize kufanya jambo hilo, kwamba uongozi wa Wasafi haukuwa na taarifa.

Amebainisha kuwa Harmonize amefanya jambo la kuhatarisha taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kumpandisha jukwaani msanii ambaye hakuwepo katika ratiba ya tamasha hilo.

“Alikuja na msanii kutoka nje na hatukujua kama alishamchukulia kibali au laa, kwa hiyo unaona kabisa anafanya vitu ambavyo vinaweza kuingiza taasisi katika tatizo,” amesema.