- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MSIGWA: TUNAANZA MIKUTANO YA HADHARA 2020 KAMA RAIS ALIVYOAGIZA
Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa amesem kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Nyasa kimesema kimevumilia na kutekeleza kwa utii mkubwa agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa hadi mwaka 2020 wakati wa kuelekea uchaguzi mkuu ambapo sasa wataanza kazi ya ujenzi wa demokrasi kama rais alivyoagiza
Kauli hiyo ameitoa jana Januari 3, 2020 mjini Iringa kwenye mkutano na Waandishi wa Habari.
Msingwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Nyasa alisema kuwa chama chake kimekuwa miongoni mwa vyama vya upinzani nchini ambavyo vilionyesha utii mkubwa wa utekelezaji wa agizo la Rais Dkt Magufuli kwa kutofanya mikutano ya hadhara kwa kipindi chote cha miaka minne sasa.
Msigwa ambaye alikuwa ameambatana na viongozi wa kanda hiyo, aliwataka viongozi wa wilaya na mikoa wa Chadema Kanda ya Nyasa kuanza kuandaa mikutano yao ya hadhara kwa kufuata taratibu zote za kuomba vibali vya mikutano hiyo ili kuendelea na ujenzi wa chama chao kuelekea Oktoba 25 siku ya uchaguzi mkuu wa Madiwani, Wabunge na Rais .
” Tuliweza kutekeleza agizo la mheshimiwa Rais kwa utulivu mkubwa japo agizo hilo halikuwa sawa maana lilikuwa ni kinyume na makuzi ya demokrasia nchini, vyama vya siasa msingi wake ni siasa hivyo kuzuia mikutano kwa haikuwa sawa lakini tuliweza kutii.
“Ila jamani si alisema hakuna mikutano ya hadhara ya vyama hadi mwaka 2020 na huu ndio mwaka 2020 hivyo tunaendelea na mikutano kama kawaida ” alisema mchungaji Msigwa .
Msigwa alisema miaka minne ambayo walizuiwa kufanya mikutano ya siasa chama hicho kanda ya Nyasa walikuwa wakijijenga zaidi kuanzia ngazi za chini.
Alisema awali hawakuwahi kuwa na misingi hiyo na kwamba kwa sasa wana mtaji mkubwa kuliko hata ilivyo kuwa mwaka 2015 walivyoingia katika Uchaguzi Mkuu .
Alisema kuzuiwa kwa mikutano ya siasa ndiko kulikowapa nguvu ya kufanya vikao vyao vya ndani na kujengana zaidi.
Alisema baada ya miaka minne bila kufanya siasa ya wazi wanatoka wakiwa na mbinu na uwezo wa kushindana vikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM).