Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 6:17 pm

MSEKWA: "SPIKA NDUGAI AMETUMIA MAMLAKA YAKE SIONI KAMA KUNAUBAYA WOWOTE"

Dar es salaam: Spika wa bunge mstafu wa Tanzania Pius Msekwa amesema kuwa haoni ubaya wowote katika utendaji kazi wa Spika wa bunge wa sasa Job Ndugai, kwa sababu utendaji huo unaendana na utawala uliopo ''Spika ametumia mamlaka yake sioni kama kuna ubaya wowote, amesema msekwa

Msekwa ameyasema hayo baada ya waandishi wa habari kumtaka atoe maoni yake juu ya uwendeshaji wa bunge wa sasa.

Msekwa amesema kuwa ingawa wakati wa uongozi wake hakukuwa na malumbano ya namna hiyo lakini hilo halimanishi kuwa Spika wa sasa anaendesha mambo kinyume na Kanuni za Bunge.

Amesema anachokifanya Spika Ndugai kinatafsiri aina ya uongozi alionao ambao siyo jambo la kushangaza kuona ukitofautiana na mfumo aliokuwa akitumia wakati akiwa katika kiti hicho. “tulifundishwa na Mzee Mwinyi(Ali Hassan) kila kitabu na zama zake.”

“Hii ni staili yake ya uongozi na ndiyo mabadiliko ya uongozi wenyewe,” amesema Msekwa wakati akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu na kurudia tena maneno hayo akisema “ ni staili yake na kila kiongozi anakuwa na mfumo wake wa kuongoza mambo.

Msekwa amesema kuwa atakuwa hajakosea lolote kama yale aliyokuwa akiyazungumza na kuyatolea maamuzi yako ndani ya Kanuni za Bunge.

Mgogoro huo umekuja baada ya mbunge wa kigoma ujiji Mh. Zitto kabwe kukosoa utendaji kazi wa bunge ambalo linaongozwa na Job Ndugai kwa kusema kuwa bunge hilo limefichwa mfukoni na muhimili mwingine, kiasa cha kufanyiwa majukumu yake. Maneno ya zitto yamekuja siku chache baada ya spika wa bunge Job Ndugai kuunda kamti ya dhahabu na kuiwasilisha moja kwa moja kwa Rais.