- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MSAJILI AKIPA SIKU 4 CHADEMA KUWASILISHA RAIBA YA KUCHAGUA VIONGOZI
Dar es Salaam. Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Tanzania amekipa siku 4 chama cha Kikuu cha Upinzania nchini Chadema Kuwasilisha mara moja Ratiba ya Mkutano Mkuu wa chama wa kuchagua Viongozi wake wa Kitaifa, Hii maana yake ni kabla ya Jumatatu Novemba 11, 2019
Barua hiyo imetolewa leo Jumatano Novemba 6, 2019 na naibu msajili wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza kwa niaba ya msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mutungi.
Kama utakumbuka Oktoba Mosi, mwaka huu chama hicho kiliandikiwa barua na ofisi hiyo ikiwataka wajieleze kwanini wasichukuliwe hatua kwa madai ya kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa kwa kuchelewa kufanya uchaguzi mkuu wa chama hicho.
Chama hicho kilijibu barua hiyo ya msajili kwa hoja sita. Katika barua hiyo msajili amesema lengo la kutaka maelezo hayo ni kurahisisha ofisi ya msajili kutekeleza majukumu yake. “Pamoja na mambo mengine, ratiba hiyo ionyeshe tarehe ya kutoa fomu za kugombea kwa wanachama wenye nia ya kugombea, tarehe ya uteuzi wa wagombea na uchaguzi.”
“Taarifa hiyo iwasilishwe ofisi ya msajili siyo zaidi ya Novemba 11 2019 saa 9:30 alasiri,” inaeleza sehemu ya barua hiyo. Nyahoza alipoulizwa kuhusu barua hiyo amesema imetolewa na ofisi ya msajili, kwamba ni mwendelezo wa barua ya Oktoba Mosi, 2019