Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 8:34 pm

MKURUGENZI TAKUKURU: UMEPEWA V8 HALAFU UNASEMA NI ZAWAIDI, TUTAKUCHUNGUZA TU

Mkurugenzi Mkuu wa Uplelezi wa Taasisi ya kuzua na kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Kassim Ephrem amesema hawataacha mwenendo wa kumchunguza mtu yeyote ambaye ataonekana anamiliki mali kuliko kipato chake cha kawaida.

Image result for mkurugenzi TAKUKURU Kassim Ephrem

Ephrem ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Kitoa cha Redio cha East Africa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast ambapo amesema ni ajabu utakuta mtu mwingine anapewa zawadi lakini anashindwa kueleza kwanini amepewa.

"Mtumishi wa umma akipewa zawadi ambayo itaonekana inazidi kipato chake, sheria inamtaka atoe taarifa kwa mabosi wake, umepewa V8 halafu unasema ni zawadi tu na kiongozi wako hukumpa taarifa tutakuchunguza tu." amesema bosi huyo wa TAKUKURU.

"Kuna kesi nyingine tumepeleka Mahakama za Mafisadi kwa kuzishtaki kampuni, na wengi wanashtakiwa kukwepa kodi au kushindwa kutumia mashine za EFD" ameongeza bosi huyo wa TAKUKURU

Ephrem amesema "walipa kodi ni wananchi ambao ni wateja wetu wakiripoti eneo fulani kuna rushwa, huwa hatumtaji kwa sababu sheria haituruhusu, ila kuna muda tunapita kutoa elimu kwa umma kuwa ukinunua kitu dai risit