- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MBUNGE LUSINDE: TUSIFANYE UCHAGUZI WA URAIS, RAIS HANA MPINZANI
Leo Bungeni Jumatatu April 9 Mbunge wa Mtera (CCM), Livingstone Lusinde ameshauri usifanyike uchaguzi mkuu wa Urais mwaka 2020 na badala yake ufanyike kwa upande wa wabunge na madiwani pekee, ili fedha zitakazookolewa katika chaguzi hiyo zitumike kutatua matatizo mbalimbali ya wananchi hapa nchini.
“Kuna faida gani kwenda kupoteza fedha chungu mzima kwa ajili ya uchaguzi Rais ambaye hana mpinzani, tufanye uchaguzi wa Udiwani na Ubunge kwenye Urais tuache na hizo pesa za uchaguzi tumkabidhi Rais zisaidie kuboresha kujenga Nchi” Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde
Lusinde ametoa hoja kwamba mpinzani wake alikuwa Lowassa kwenye Uchaguzi wa mwaka 2015 aliyepata kura milion 6 na sasa yupo CCM ambaye ameshaziunganisha na kura milioni 8 alizopata Rais Magufuli "kwasababu tumeona, hata mshindi wa pili aliyepata kura milioni 6 ameonganisha na milioni 8, kwahiyo ndgugu zangu minataka kuwashauri , mitandao yote, wanazuoni wote hoja hii naiweka mezani" amesema Lusinde