- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAKALA: WANAWAKE WA INDIA HAWAJAWAHI KUWAITA MABWANA ZAO KWA MAJINA
INDIA: Mamiloni ya wanawake nchini India hawajawai kuwaita mabwana zao kwa majina yao ikiwa ni njia ya kuwaheshimu.
Tamaduni hiyo inaheshimika zaidi vijijini licha kutokuwepo sana mijini.
Sasa waendesha kampeni wanawashauri wanawake vijijini paa nao waachane na tamaduni hiyo.
"Wazazi wangu walioana kwa miaka 73 hadi babangu alipoaga dunia mwaka uliopita.
Wakati wa harusi yao, mama yangu alikuwa na umri wa chini ya miaka 11 na babangu alikuwa amehitimu miaka 15.
Katika miaka hiyo yote waliishi pamoja katika kijiji kidogo kwenye jimbo lililo kaskazini mwa India la Uttar Pradesh, hakumuita kwa jina lake hata siku moja.
Alipokuwa akizungumza na sisi alimuita baba kwa jina "babuji" ambalo humaanisha "baba" ambalo tulilitumia. Alipokuwa akimuiti moja kwa moja alitumia jina "Hey ho" linalomanisha "wewe".
Tukiwa wadogo tulipata kufahamu hilo na tukaanza kumfanyia mzaha. Tulijaribua kumtega ali aweze kutamka jina la baba hata mara moja, lakini kamwe hakulitamka", mwanamke mmoja alisema.
Kwenye utamaduni wa India, bwana ni sawa miungu na kuanzia umri mdogo wanawake hufunzwa kumheshumua.
Anaambiwa kuwa kumuita kwa jina inaweza kumletea bahati mbaya na kupunguza maisha yake, na kuivunja tamaduni yaweza kumletea mwanamke adhabu kali.
Mwanamke moja katika jimbo la Orisa aliadhabiwa vikali.
"Siku moja mkwe wangu aliuliza kuhusu ni nani alikuwa ameketi nje, niliwataja kwa majina wanaume wote waliokuwa akiwemo mjomba wa mme wangu," anasema Malati Mahato.
Mkwe wake alilalamika kwa baraza la kijiji lililoamua kuwa Mahato alifanya makosa makubwa na kumuadhibu na watoto wake kwa kuhamishwa kwenda nyumba ili kando kabisa mwa kijiji. Kwa muda wa miezi 18 hajachanganyika na watu wengine kijijini.