- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAKALA: JE, MAMA ANAYENYONYESHA MTOTOANAWEZA KUPATA MIMBA ?
Katika miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua, mwanamke anayenyonyesha mtoto anapata kinga ya mimba kwa asilimia kubwa. Lakini inabidi mama anyonyeshe mtoto kwa kipindi kirefu (muda wote mtoto awe ananyonya maziwa ya mama tu na anyonye kila anapohitaji) na vilevile mama awe hajaanza kupata hedhi yake. Kama mama ameanza kupata hedhi yake au kama anampa mtoto chakula kingine, anaweza kupata mimba tena. Kwa hivyo, anashauriwa kutumia njia za kupanga uzazi i i ili kuzuia mimba za mfululizo.
Wakati wa kutunga mimba ni mbegu moja tu ya kiume inayopenya kwenye yai, mbegu nyingine zinaenda wapi?
Ni kweli kwamba wakati wa kujamii au kutunga mimba ni mbegu moja tu ya kiume i inayopenya kwenye yai. Mbegu zilizosalia hufa na kutoka kwa kupitia ukeni kwa sababu hazina kazi tena. Inashauriwa kwamba watu wanapomaliza kujamii ana, wasafishe vizuri sehemu zao za uzazi.
Je, ni madhara gani atapata mama mjamzito endapo atajamiiana na mwenzi wake?
Kama kati ya mwanamke na mwanaume hakuna mwenye magonjwa ya zinaa, hakuna madhara yoyote kwa mwanamke mwenye mimba kujamii ana na mwenzi wake. Mfuko wa mimba hufunga kabisa na kifuko kinamzunguka mtoto vizuri, na hivyo hakuna uwezekano wowote wa mbegu za kiume kupenya na kumfikia mtoto.Inashauriwa lakini wakati wa kujamii ana na mwanamke mjamzito tumbo lisigandamizwe sana. Wanawake wengine hawana hamu kubwa ya kujamii ana hasa mwishoni mwa ujauzito, na mwanaume anashauriwa kuheshimu hisia hizi za mwanamke.
Kama mwanaume atakuwa ameambukizwa magonjwa ya zinaa wakati wa kujamii ana, hii i ii inaweza kuwa hatari sana kwa mwanamke na pia kwa mtoto tumboni. Wakijamii ana mume na mke wakati wa ujauzito, lazima wawe na uhakika kwamba hamna mwenye magonjwa ya zinaa au watumie kondomu kwa ajili ya kinga. Iwapo watakuwa na wasiwasi wowote, wamwone daktari kwa uchunguzi