- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAJALIWA : MARUFUKU KUJINGA VIWANDA MAENEO YA SHULE
Dar es Salaam. Waziri Mkuu nchini Tanzania, Kassim Majaliwa amepiga marufuku shughuli zote ambazo hazihusianai moja kwa moja na taaluma kama vile uwepo wa viwanda Kujengwa karibu na maeneo ya shule, lengo ili kutoa fursa kwa wanafunzi kuwa kwenye mazingira mazuri ya kujifunzia. “Sheria inakataza kuweka matumizi yoyote yasiyokuwa ya kitaaluma katika maeneo ya shule kwani yanasababisha kelele hivyo wanafunzi kushindwa kusoma vizuri,” amesema.
Waziri Mkuu aliyasema hayo jana jioni Jumanne Machi 3, 2020 baada ya kupokea malalamiko ya wazazi kuhusu eneo la shule ya msingi Mshikamano iliyoko Halmashauri ya Mji Handeni kuuzwa kwa mfanyabiashara ambaye amefungua karakana ya kutengeneza magari.
Kufuatia hali hiyo, Majaliwa ameuagiza uongozi wa halmashauri hiyo ukazungumze na mfanyabiashara huyo ili aondoe karakana katika eneo hilo na kumtafutia eneo mbadala kwa ajili ya kuendesha shughuli zake na eneo hilo libaki kwa ajili ya masuala ya kitaaluma.
Pia, Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa Halmashauri ya Mji wa Handeni upange matumizi bora ya ardhi kwa kuainisha maeneo ya makazi, biashara, viwanda na huduma za kijamii ili kuepuka mji huo kujengwa bila ya mpangilio.