Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 5:40 am

MAHUSIANO: JE , UNAJUA NI NINI MWANAUME ANATAKA KWENYE MAHUSIANO?



Tukiacha faragha ,chakula kizuri,usafi na mambo mengine mengi ,wanaume wana mambo yanayowavutia kwa wanawake,vipo vitu wanaume wanavutiwa navyo kwenye mahusiano au ndoa zaidi ya vile wanawake wengi wanavijua kama kuvaa vizuri kuwa na umbo la mvuto na mengine mengi. Ila wacha nikupe ubuyu juu ya mambo mengine muhimu wanaume wanataka kuona kutoka kwa mwanamke.

Kujiamini

Wanaume wanapenda sana mwanamke anaejiamini na kujisimamia, Mwanamke mwenye msimamo maradufu, anaejua nini anafanya na kujielewa anaeweza kufanya mambo yake bila kumganda kila wakati. Wanawake wengine wanadhani kupenda basi ndio kuwa pale kila saa, kila wakati hapana kuna wakati kila mtu anatakiwa ajichanganye na marafiki au ndugu bila wewe kuwepo.

Uhuru

Wanaume hawapendi kufwatiliwa hata kama yeye anafanya kitu kama hicho kwako, uko wapi? unafanya nini? uko na nani ? wanaume wanataka mwanamke ambae sio kizuizi katika mambo yao, kwahiyo kwa wale wadada wanaopenda kufwatilia wanaume zenu mnakosea, wapeni uhuru japo sio sana, ila itasaidia hii pia itawafanya wajisikie huru kwenye mahusiano. Na muache basi awe yeye wa kwanza kukutafuta wakati mwingine, sio kila dakika sms, dakika simu ina waboa sana.

Kuhudumiwa

Hata kwa vitabu vya dini vinasema mwanamke ni msaidizi kwa mwanaume hii ndio maana wanaume Bado wana tabia za kupenda kuhudumiwa, atalelewa na mama yake atalelewa na mke, hii ni kawaida mwanaume atakusaidia kazi azipendazo ila huwezi mlazimisha afanye kila kitu, basi kama unajua nini mpenzi wako anataka fanya atakavyo,kuwa msaada pale anapohitaji. Hapa siongelei kufuliwa na kusaidiwa kazi za ndani tu,sababu hiyo peke ake sio dawa ya mwanaume kukupenda, ila unajua kumuhudumia mwanaume au “How can you handle a man” kuwa mwanamke anayejua nini mwanaume anataka. Tumia muda wako kumsoma mwenza wako.

Mawasiliano

Ninaposema mawasiliaono namaanisha “communication” wanawake wengi wanapenda kuwaacha wanaume wao waseme nini wanataka, au wanataka mwanaume aotee nini anataka bila yeye kumwambia, usione soo, kusema unachotaka kuwa muwazi na sema utakacho “be straight” wanaume hawapendi michezo ya kijinga “love Games” au tunaita “Drama” drama zikizidi zinawakimbiza wanaume. Hii ni moja kati ya sumu kubwa sana kwenye mahusiano.