Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:38 am

MAHAKAMA KENYA YASEMA NI RUKRA KUENDESHA GARI UKIWA UMEKUNYWA POMBE

Mahakama ya Kiambu nchini Kenya imetoa hukumu ikieleza kuwa kuendesha gari huku ukiwa amekunywa pombe sio kosa kama unaweza kukidhibiti chombo hicho cha moto kiwe gari, matatu(Daladala), Pikipiki na vinginevyo

Related image

Kwamujibu wa Hakimu Mwandamizi, Bryan Khaemba ametoa maelezo hayo katika hukumu iliyomuachia huru mshtakiwa wa kosa la kuendesha Pikipiki akiwa amelewa
Mahakama hiyo imeamua kuwa, ili mtuhumiwa awe na hatia, inapaswa muendesha mashtaka kutoa ushahidi usioacha shaka kuwa mtu huyo hakuwa na uwezo wa kudhibiti chombo hicho cha moto

Askari Polisi aliyetoa ushahidi katika kesi hiyo, aliiambia Mahakama kuwa mtuhumiwa aliwashinda nguvu yeye na askari wenzake wawili walipotaka kumkamata

Maelezo hayo ndiyo yaliyomuokoa mshtakiwa, kwani Mahakama iliamini mtu aliyewashinda watu watatu, hata kama alikuwa amekunywa pombe hawezi kushindwa kudhibiti mwendo wa Pikipiki yake