- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
MAHAKAMA IMEWAFUTIA MASHTAKA WALIOJIUNGANISHIA MOMBA LA MAFUTA
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewafutia mashtaka na kuwaachia huru watuhumiwa 5 waliokuwa wanakabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia kiharamu bomba la mafuta la Mamlaka ya Bandari (TPA).
Uamuzi huo Umefikiwa leo Septemba 23 kufuatia DPP kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.
Washtakiwa hao 5 akiwemo aliyekuwa mfanyakazi wa bomba la mafuta la Tazama, Samwel Nyakirang’ani miaka 63, wamefutiwa mashitaka na Hakimu mkazi mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Thomas Simba.
Washtakiwa wengine ni pamoja na Mwalimu wa Shule ya Msingi ya Ufukoni, Nyangi Matoro miaka 54, Mfanyabiashara Farijia Ahmed miaka 39, Malaki Mathias miaka 39, Kristomsi Angelusi miaka 25, Henry Fredrick miaka38 na fundi ujenzi Pamfili Nkoronko miaka 40.
Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya Uhujumu uchumi ya kujiunganishia isivyo halali katika bomba la mafuta ya Dizeli ambapo imedaiwa, washtakiwa wote katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2015 na Januari 8, 2018 mwaka huu, huko maeneo ya Tungi Muungano katika Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam walijiunganishia bomba la upana wa inchi moja kwenye bomba la inchi 24 la diesel material yasiyoshika kutu bila kuwa na kibali cha Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Pia katika tarehe na maeneo hayo hayo, washtakiwa kwa pamoja walitoboa na kuharibu bomba la Inchi 24 linalotumika kusambaza mafuta ya Dizeli mali ya TPA na kati ya 2015 na January 8, 2018 maeneo ya Tungi Kigamboni, walitoboa bomba la inchi 28 la mafuta linalotumika kwa ajili ya usambazaji wa Crude Oil likiwa ni mali ya TPA.