November 26, 2024, 4:42 am
- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
LUGOLA " MARUFUKU POLISI KUPIGA FAINI BODABODA NA BAJAJ YA HAPO KWA PAPO"
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amepiga marufuku Polisi wote nchini wa Usalama Barabarani kuwalipisha faini waendesha bajaji na bodaboda papo kwa papo wanapofanya makosa barabarani na kutaka wapewe siku saba kama ilivyokuwa kwa magari.
Kauli hiyo ya Lugola ameitoa Leo Agosti 3, 2019 akizungumza na mamia ya Wamiliki na Waendesha Bajaj na Bodadoda Mkoawa Kilimanjaro, katika mkutano uliofanyika Ukumbi wa CCM, Mjini Moshi, Mkoani humo, ukihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Dkt. Anna Mghwira.