- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
LHRC : BADO HAKUNA TAARIFA WAPI ALIPO TITO MAGOTI
"Pamoja na Polisi kusema wanaye TitoMagoti kwa "Mahojiano na Uchunguzi" hawajatoa taarifa za kituo gani anafanyiwa mahojiano hayo na kwa kosa gani. Magoti na wenzake (kama wapo) wanayo haki ya kupata wanasheria kwa mujibu wa Sheria za Tanzania," Bi Henga amechapisha hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter.
Magoti alikamatwa Jana Ijumaa Dec 20, 2019 asubuhi jijini Dar es Salaam na watu ambao walikuwa wamevaa kiraia na kuzuka taharuki kuwa ametekwa na watu wasiojulikana.
Shirika la Habari la BBC Ijumaa iliongea na Mambosasa juu ya kushikiliwa kwa Tito Magoti hata hivyo hakueleza zaidi ni tuhuma zipi zinazomkabili Tito na wenzake na kusema "kwa sasa uchunguzi unaendelea na tuhuma hizo hazijatajwa kwa sababu maalumu".
Kwa mujibu wa Bi Henga, hata baada ya polisi kuthibitisha kumkamata Tito, walienda Kituo Kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam lakini hawakumkuta ofisa huyo.