Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:27 pm

LAZARO NYALANDU: TULIVAMIWA NA WATU WENYE SILAHA KALI, WAKATUMRISHA TUONDOKE

Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania Lazaro Nyalandu ametoa ufafanuzi juu ya tukio la kuvamiwa kwenye mkutano wa Ndani na Watu wenye silaha kali mnamo tarehe 27 Mei 2019.

Nyalandu amesema kuwa walikwenda kijijini Itaja, Wilayani Singida kuongea na VIONGOZI wa vijiji na vitongoji Kata ya Itaja kuhusu zoezi linaloendelea nchi nzima la chama cha Demkrasia na Maendeleo CHADEMA la kuwatambua na kuwaandikisha wanachama wao wapya.

Anasema kuwa wakati wapo kwenye kikao hicho cha ndani walivamiwa na watu ambao hawakuwa wakiwafahamu na wakawataka waondoke nao bila kuhoji

"kikao chetu cha NDANI, kilivamiwa na watu ambao hatukuwafahamu, wakiwa na silaha na kuamrisha mimi, pamoja wenzangu wawili (David Jumbe na Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya Itaja, ndugu Peter) tuondoke nao" amesema Nyalandu kupitia Ukurasa wake wa Instagram.


"SOTE tulipatwa na mshtuko mkubwa, na hatukupewa utambulisho wala sababu ya kutolewa kwenye kikao na kuchukuliwa na watu wenye silaha mithili ya wahalifu na kutiwa nguvuni, huku wote tuliokuwa nao wakiwa wamepigwa bumbuwazi."

Nyalandu alijiuzulu Nyazifa zake zote ndani ya CCM tahere 30 Oktoba 2017 Na kujiunga na CHADEMA, amabapo kabla ya maamuzi hayo ya kujiuzulu alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini alisema amechukua uamuzi huo wa kujiuzulu kutokana na kutokuridhishwa na mwendo wa siasa nchini Tanzania, ukiukwaji wa haki za kibinaadamu, ongezeko la vitendo vya kidhalimu dhidi ya raia na kutokuwepo kwa mipaka baina ya mihimili ya dola - Serikali, Bunge na Mahakama.

Nyalandu amesema kuwa Walimchukua kila moja wetu katika chumba tofauti na kutuhoji juu ya UHALALI wa Kikao hicho cha CHADEMA, na kudai kuwa kulikuwa na HARUFU ya rushwa. Baada ya mahojiano, walitupeleka katika kituo kikuu cha Polisi Singida, na muda mfupi baadae tukasikia taarifa ya TAKUKURU Singida kuwa wao wamejiridhisha hapakuwa na tatizo na wametukabidhi mamlaka ya Polisi.

"Polisi walitufanyia mahojiano mengine, kila mmoja wetu katika chumba tofauti, na kutujulisha kuwa wao hawakuwa na neno lolote juu yetu, isipokuwa yatupasa tutoe taarifa kwa OCD Singida.

Tulipopewa dhamana usiku huo, ilikuja AMRI KUTOKA JUU kwamba dhamana hiyo ifutwe, na tukalazwa katika rumande ya Central Police.

''UONEVU ni dhambi mbele za Mungu, na wanadamu.''

CHADEMA na Vyama vingine vyote vya Upinzani wamewekwa katika hali ya mashaka na mateso, na tunatishiwa usalama wetu, na kuwekewa mipango LUKUKI ya kututungia na KUTUBAMBIKIZIA kesi.

Hakika, HAKI huinua TAIFA, na WOTE wenye MAMLAKA, waone fahari kutenda MEMA. Kwa nilichokipitia siku hizi chache, nawasihi sana CHADEMA, na UPINZANI kwa ujumla wake, SIKU tutakapo shinda na kushika DOLA, tusiwafanyie wana CCM au watu wengine mateso kama haya, kwakuwa, yatupasa tuushinde UBAYA kwa WEMA." aliongeza Nyalandu