Home | Terms & Conditions | Help

September 8, 2024, 8:13 am

KOREA KUSINI IMEVUNJA MKATABA WA KUPEANA TAARIFA ZA KIJASUSI NA JAPAN

Korea kusini imeamua kusitisha makubaliano ya kubadilishana taarifa za kijasusi na Japan ambayo kimsingi yalianzishwa ili kubadilishana taarifa juu ya shughuli za uzalishaji wa nyuklia na makombora ya Korea kaskazini.

Image result for south korea and japan conflict

Mahusiano baina ya nchi hizo mbili yalianza kuharibika Oktoba mwaka jana wakati mahakama kuu ya Korea kusini ilipoyaamuru makampuni ya Japan kulipa fidia watu ambao ni wahanga wa kufanyishwa kazi kwa nguvu wakati wa utawala wa kikoloni wa Japan katika rasi ya Korea kati ya mwaka 1910 na 1945.

Image result for Military conflict between Japan and South Korea

Uamuzi huo wa mahakama ulifikia katika mzozo wa kulipizana kisasi kibiashara hali ambayo iliongeza kuporomoka kwa mahusiano hayo. Katika tangazo lake leo la kusitisha makubaliano hayo, ofisi ya rais wa Korea kusini imesema vikwazo vya kibiashara vya hivi karibuni vilivyowekwa na Japan vimeharibu zaidi uaminifu kwa pande hizo mbili.