Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 10:57 pm

KILA MWANAFAMILIA AJALI YA NDEGE UKRAINE KUPEWA MILIONI 45 KILA MMOJA

Waziri Mkuu wa Canada Bw. Justin Trudeau amesema kuwa watatoa fidia ya Dolla $19,200 sawa na Shiling milioni 45 kwa kila mwanafamilia raia au mkazi wa Canada aliathirika na Ajali ya ndege ya Ukraine Airlines.

Image result for Justin Trudeau and ukraine airlines crush"

Raia wapatao 57 kutoka nchini Canada walikuwemo kwenye ndege hiyo baada ya kuangushwa na Makombora ya Iran.

Kuanguka kwa ndege hiyo kulitokea saa chache baada ya Iran kushambulia kambi za kijeshi za Marekani nchini Iraq kwa makombora ya masafa marefu.

Vyombo vya habari vya Marekani vinaashiria ndege hiyo ilidhani kuwa ndege ya kivita ya Marekani wakati Iran ilipokuwa ikijiandaa kujibu mashambulio dhidi ya Marekani baada ya wao kushambulia vituo vyake vya kijeshi nchini Iraq kwa makombora.

Kituo cha habari cha CBS imevinukuu vyanzo vya kijasusi vya Marekani vinavyodai kuwa picha za satelaiti zinaonesha mwanga wa makombora mawili ambao ulifuatiwa na mwanga wa mlipuko.

Image result for Justin Trudeau and ukraine airlines crush"

Kituo cha habari cha CBS imevinukuu vyanzo vya kijasusi vya Marekani vinavyodai kuwa picha za satelaiti zinaonesha mwanga wa makombora mawili ambao ulifuatiwa na mwanga wa mlipuko.

Kanda ya video iliyopatikana na New York Times ilionenesha jinsi makombora yalivyokuwa yakipita katika anga la Tehran na baadae kulipuka ilipokutana na ndege.

Karibu sekunde 10 baadae mlipuko mkubwa ulisikika ardhini. Ndege iliyoshika moto, inaendelea kupaa.

Rais wa Marekani Donald Trump siku ya Alhamisi alisema: "nina mashaka" juu ya (kuanguka) kwa ndege. "Inawezekana kuna mtu amefanya kosa kubwa."

Iran imetangaza kutokabidhi kisanduku cheusi cha kuhifadhi taarifa za ndege kwa kampuni ya ndege ya Boeing ama serikali ya Marekani kwa uchunguzi wa ajali hiyo.

Hatua hiyo inatokana na mzozo uliokomaa baina ya Marekani na Iran, hasa baada ya Trump kuagiza shambulio la anga lililomuua Jenerali wa Iran Qasem Soleimani Januari 3.

Chini ya sheria za kimataifa za usafiri wa anga, Iran ina haki ya kuongoza uchunguzi wa ajali hiyo lakini kawaida huwa kampuni iliyotengeneza ndege pia hushirikishwa kwa karibu.

iranHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMaombolezo yameendelea ,kuwaomboleza wafanyakazi wa ndege hiyo,kwenye jumba la makumbusho yaliyoko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kyiv's, Boryspil

Ndege hiyo ni Boeing 737-800 ambayo imetengenezwa Marekani, nchi ambayo ni hasimu wa Marekani.

CBS na Newsweek waliripoti kuwa maafisa wa ujasusi wa Marekani na Iraq wana hakika kuwa ndege hiyo iliangushwa na makombora ya Iran.

CBS wamechapisha taarifa inayodai kuwa mitambo ya rada ya Marekani ilibaini makombora mawili yakirushwa muda mfupi kabla ya ndege hiyo kulipuka.Kwa upande wa Newsweek wamewanukuu maafisa wa Marekani na Iraq ambao wanaamini ndege hiyo ilidunguliwa na makombora ya Kirusi aina ya Tor M-1 ambayo Nato huyaita Gauntlet.

Maafisa wawili kutoka makao makuu ya jeshi la Marekani wameithibitishia Newsweek kuwa shambulio hilo lilikuwa la bahati mbaya.