Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:26 am

JESHI LA POLISI: NIMARUFUKU KUKUSANYIKA BAA NA FUKWE ZA BAHARI.

Dar es salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku kufanya mikusanyiko yeyote katika fukwe za bahari na kwenye baa katika kipindi chote hiki cha sikukuu za pasaka.

Marufuku hiyo imetolewa leo Alhamisi Aprili 9, 2020 na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa na kuwataka wananchi wote kuepuka mikusanyiko isiyokuwa ya lazima na kuendeleza na jitihada za kujikinga na virusi vya corona.

“Katika kipindi chote cha pasaka polisi Kanda Maalum imejipanga hukakikisha hakuna uhalifu, vurugu na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima inafanyika ikiwa ni maelekezo ya Serikali ya kujikinga na maambukizi ya corona,” amesema Mambosasa.

Vilevile, jeshi hilo limewataka madereva wa pikipiki walioruhusiwa kuingia katikati ya jiji kufuata sheria kwa kuvaa kofia ngumu na kuacha kupita barabara zilizokatazwa.
Aprili Mosi, 2020, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliruhusu bodaboda na bajaji kuingia katikati ya jiji ili kupunguza kero ya usafiri uliotokana na daladala kutakiwa kupakiwa abiria kulingana na idadi ya viti ‘level seat’.

“Fursa waliyoipata wataipoteza wenyewe wameruhusiwa wanakuja na tabia zao za kuendelea kukiuka na kuwa wakaidi, tumejipanga vizuri kuhakikisha kwamba yeyote atakayeenda kinyume tunamchukulia hatua,” amesema
“Tunawashukuru waliotii agizo la Serikali la kupakia abiria kulingana na idadi ya viti vilivyopo ndani ya gari (level seat) kwa watakaokaidi agizo hilo sheria itafuata mkondo wake.”

Ameongeza kuwa jeshi hilo limejipanga vizuri
kwa kutumia doria za askari wa miguu, magari, pikipiki, mbwa na farasi kuhakikisha maeneo yote yanakuwa salama.