Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:39 pm

JAJI MKUU: RAIS HUWA ANASHAURIWA NA TUME YA UTUMISHI YA MAHAKAMA

Dar es Salaam. Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amesema Tume ya Utumishi wa Mahakama ndiyo tume pekee iliyopewa mamlaka ya kumshauri Rais wa Tanzania kuhusu mambo mbalimbali ambayo miongoni mwa mambo hayo ni kumshauri kuhusu uteuzi wa Jaji Kiongozi na majaji wa mahakama kuu.

Image result for rais magufuli na prof juma"

Profesa Juma amesema hayo leo Jumatatu Februari 3, 2020 katika wa hafla ya kuwaapisha viongozi mbalimbali wakiwamo makamishna wa tume ya utumishi wa mahakama.

Prof. Juma amesema ni vizuri wananchi kurejea katiba ya nchi ili kujua masuala hayo ambayo baadhi hawayajui.

“Tume hii ndiyo vilevile imeshiriki katika kupendekeza uteuzi wa mtendaji mkuu wa mahakama, msajili mkuu, msajili wa mahakama ya rufani na msajili wa mahakama kuu,” amesema. Amefafanua kuwa tume hiyo pia imepewa jukumu la kumshauri Rais kuhusu masuala ya nidhamu ya majaji wa rufani, mahakama kuu na watumishi wote wa mahakama.

Image result for rais magufuli na prof juma"

“Vilevile tume hii ina umuhimu katika masuala ya maslahi ya watumishi wote wa mahakama, sisi ndio huwa tunamshauri Rais kwa hiyo tume hii ina uzito sana,” amesema. Amebainisha kuwa tume hiyo imeundwa kikatiba na yeye ni mwenyekiti, Jaji Kiongozi wa Tanzania, Dk Eliezer Feleshi na wajumbe wengine.

Awali, Rais Magufuli aliwaapisha viongozi mbalimbali wakiwamo makatibu wakuu, makatibu tawala wa Mikoa, viongozi wa mahakama, kamishna ya ardhi, makamishna wa tume ya utumishi wa mahakama na viongozi wa makundi mawili ya vyombo vya ulinzi na usalama