- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
IMF: UCHUMI WA DUNIA UNATARAJIWA KUPOROMOKA KAMA MWAKA 1929
Mkuu wa Shirika la Fedha la Duniani (IMF), Bi Kristalina Georgiaieva, amesema jana la ugonjwa wa corona Duniani litasababisha "athari mbaya zaidi za kiuchumi kama ile iliyoteka mwaka 1929 kabla ya vita vya pili vya Dunia.
Kristalina Georgieva ameonya kuwa ukuaji wa uchumi duniani utaanguka kabisa katika mwaka huu wa 2020 huku 170 kati ya nchi wanachama 180 wa IMF zikishuhudia kupungua kiwango cha mapato ya wastani.
Nchi nyingi kwa sasa ziko hatarini kuathirika kiuchumi kiutokana na ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya Corona.
Wakati idadi ya vifo inakaribia kufikia 100,000 kutokana na ugonjwa wa Covid-19, Jumuiya ya kimataifa inatafuta jawabu la pamoja la kiuchumi na kidiplomasia kuhusu janga hilo, ambalo linatishia ulimwengu kwa kiasi kikubwa.
Zaidi ya watu 94,000 wamefariki dunia baada ya kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19.
Takwimu zingine za kutia moyo barani Ulaya na Marekani zinatoa matumaini ya kupungua idadi ya vifo katika siku za usoni ikilinganishwa na ile iliyotangazwa awali. Kwa mara ya kwanza, idadi ya wagonjwa katika wodi ya wagonjwa mahututi wa Corona imepungua nchini Ufaransa, na wagonjwa wa Corona wanaendelea vizuri nchini Marekani.
Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa amezitaka serikali kuchukua hatua zaidi za kusaidia makampuni ya kibiashara ili kuepusha athari kwa uchumi na kufanya iwe vigumu kuufufua baada ya janga hili kumalizika.
Wiki ijayo kutakuepo na mikutano kati ya IMF na Benki ya Dunia, ambayo itaandaliwa kwa njia ya video kutokana na vizuizi vilivyowekwa kutokana na COVID-19.