Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 5:49 am

IGP SIRRO: WATU WA MITANDAONI NI SUMU SANA, TUWASHUGHULIKIA WANAOPOTOSHA

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Simon Sirro ameahidi kuwashughulikia watu wote wanaotumia mitandao yao ya kijamii vibaya kwa lengo la kutoa takwimu zisizo sahii juu ya ugonjwa wa Corona(Covid-19) nchini.

IGP SIRRO AWAONYA WALIOPATA MSAMAHA WA RAIS SIKUKUU YA MUUNGANO ...

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo Aprili 25, 2020 na kuwataka Makamanda wote wa mikoa nchini kuwashughulikia kikamilifu watu hao kwa mujibu wa Sheria za nchi.

“Watu wa mitandao ni sumu sana…hasa wanapoitumia vibaya…maelekezo kwa makamanda hawa ni kuhakikisha kwamba akijitokeza mtu mmoja au kikundi cha watu wakafanya haya wanayoyafanya kwa ajili ya kuwaletea watanzania hofu…tuwashughulikie vizuri sana…” - amesema IGP Sirro.

Sirro ameongeza kwa kusema kuwa hakuna kitu kibaya kama uvumi," na uvumi ndio unaleta hofu, na hofu ikishamuingia binaadamu hata tiba akipa hawezi pona vizuri"

Hatua hiyo ya IGP Sirro ni kufuata maelekezo aliyopewa Aprili 22, 2020 na mkuu wa nchi wa Tanzania Rais John Magufuli aliyemtaka kushughulika nao watu wote wa mitandaoni wanaopotosha na kuwajaza hofu wananchi juu ya ugonjwa wa corona "Hofu zinajengwa na maadui kwa makusudi yao…niwaombe wanaotumia mitandao wajizuie kuongea uongo…IGP uko hapa…shughulika nao…hawa ni saizi yako….’alisema Rais Magufuli.