Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 9:55 am

HIZI HAPA DALILI ZA UJAUZITO[MIMBA].

Mpaka sasa hakuna kipimo ambacho kinaonyesha moja kwa moja kama ujauzito (Mimba) umeingia mpaka kusubiri kwa mda wa siku 7 mpaka 10 baada ya mbegu za kiume kukutana na yai (Urutubishaji) . Ndani ya siku hizo ndipo ujauzito huweza kupandikizwa. Baada ya mimba kupandikizwa ndipo kiinitete (Embriyo) huweza kutoa Human Chorionic Gonadotropin kifupi huitwa hCG. Na hiyo homoni ikishaachiwa kwenye palcenta ndipo dalili za ujauzito huonekana.

Hizi zifuatao ni dalili10 za ujauzito.

1. Kukosa mzunguko wa hedhi (Peridod)

Hii ndio dalili kubwa ambayo watu wengi huijua wakati mwingine mtu anaweza akakosa period ndani ya mda unaotakiwa kutokana na sababu za kiafya, mazingira au hata mawazo akaanza kufkiria kuusu ujauzito sababu kukosa mzunguko ni dalili mojawapo ya ujauzito. Ingawa wakati mwingine mtu anaweza akawa mjamzito lakini akaendelea kupata period kipindi cha mwanzo.

2. Homa za asubuhi

Mara nyingi hizo homa za asubuhi huwa kipindi cha miezi mitatu ya kwanza (first trimester) ingawa pia baadhi huendelea hadi second trimester (miezi mitatu ya pili). Ila wakati mwingine hizi homa za asubuhi huja kutokana na sababu za ulaji.

3. Mabadiliko ya matiti na chuchu

Mwanzo pia unaweza ukaona mabadiliko ya matiti ambayo ni kama:-

  • Matiti kuuma au kuvimba (Au vyote kuuma na kuvimba).
  • Chuchu kubadilika rangi.
  • Chuchu husisimka zinapoguswa.
  • Unaweza ukaona mishipa ya damu kwenye maziwa.
  • Sehemu ya chuchu kuongezeka ukubwa.

4. Ute ute kuongezeza ukeni

Kuwepo kwa ute mwingi mwingi kwenye uke. Baadhi ya wanawake hupata kidogo ila baadhi hupata mwingi kiasi cha kuwabugudhi.

6. Uchovu

Pindi unapopata ujauzito mfumo wa umeng`enyaji chakula huongezeka ili kukidhi mtoto na mama na hapo ndipo uchovu hutokea. Kama utajisikia kulala inabidi ulale bila kujizuia.

7. Kukojoa mara kwa mara

Wiki moja baada ya kutunga mimba mjamzito huenda haja ndogo mara kwa mara lakini hutoa mkojo kidogo sana. Hali hii hutokea sababu kiini huanza kutoa kemikali ya hCG.

8. Kuchukia au kupenda baadhi ya harufu

Wakati mwingine mjamzto hupenda hata harufu mbaya. Na baadhi ya harufu ambazo ulizipenda kabla hapa utaanza kuzichukia.

9. Kutokea kwa Pimpozi na chunusi

Hutokea kipindi cha mwanzo cha ujauzito. Pindi zikitokea usizitoe wala kuzitumbua sababu zitaacha madoa kwenye uso wako.

10. Kubadilika kwa rangi ya uke

Kutokana na kuongezeka kwa damu sehemu za fupanyonga basi husababisha uke kuwa na rangi ya uzambarau kuliko kawaida.

Hitimisho

Unashauriwa baada ya kuona badhi ya dalili hizo ni vizuri kusubiri mpaka muda muafaka wa ujauzito kuonekana (siku 7 hadi 10) na uende kupima.