Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 3:32 am

FAHAMU WALICHO KIANDIKA MASTAA NA WANASIASA LEO SIKU YA PASAKA

Dar es salaam: inakumbukwa kuwa juma pili ya Tarehe 16 ya mwezi April ndio siku ya Pasaka siku ambayo kwa wakristo wanaamini ndio siku ya kufufuka kwa mkombozi wao YESU KRISTO, sasa wapo mastaa na wanasiasa ambao wameonyesha hisia zao juu ya siku ya leo ya PASAKA, ambao wengi wao wametoa hisia zao na salamu zao kupitia mitandao ya kijamii ,

Mwingulu nchemba: huyo ni waziri wa mambo ya Ndani wa Tanzania yeye ameandika jana kwenye ukurasa wake wa Instagram "mimi na familia yangu tunapenda kuwatakia PASAKA njema watu wote zaidi wakristo waote ulimwenguni kote, tunapokumbuka kuteswa na kufufuka kwa mwana wa mungu anaye ishi na kumiliki -YESU KRISTO"

John mnyika: huyu ni naibu katibu mkuu bara naye alindaika katika ukurasa wake wa instagram "Amefufuka kaburini hayumo. Niukombozi wetu. napenda kuwatakia siku kuu njema ya pasaka na mapumziko mema."

Rais Dr. John pombe magufuli Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwenye ukurasa wake wa Twitter alitwet " Nachukuwa nafasi hii kuwatakia heri ya pasaka watanzania wote. mafunzo tunayo yapata juu ya mateso, kifo na ufufuko wa yesu kristo yaendelee kuimarisha Umoja na utaifa wetu.........."

JOTI: huyu ni komediani mahiri Tanzania Yeye aliandika kwenye .ukurasa wake wake wa Instagram huku akiweka picha ya kuku wakiwa wanaelekezwa kuchinjwa akasema kuwa " kipindi hichi hawa viumbe wanapoteza uhai sanaaa, pasipo kujua kuwa wanafamilia zao... Hebu viongozi wa serekali kupitia (KAMANDA WA POLICE) tushirikiane kwa pamoja tutafute mcheleili tuone tunafanyaje"

Reginald Mengi: mwenyekiti wa IPP Media aliandika kwenye Ukurasa wake wa Twitter "My Twitter friend I Greatly Value our connection through twitter. I wish you blessed Easter holiday, full of happiness, love and lots of fun.