- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
FAHAMU UGONJWA WA KISONONO, DALILI NA TIBA YAKE.
KISONONO ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao hukua na kuzaliana kwa haraka katika sehemu zenye unyevunyevu na joto mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa wanawake (cervix), mirija ya kupitisha mkojo au shahawa (urethra), mdomoni na kwenye puru.
Maambukizi mengi kwa wanawake hutokea kwenye shingo ya kizazi (cervix). Asilimia 75 ya ugonjwa wa gono hutokea kwa watu wenye umri wa miaka 15 – 29, wanawake walio katika umri wa miaka 15 -19 na wanaume walio katika umri wa miaka 20 – 24 wako kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.
Ugonjwa huu huambukizwa vipi?
Ugonjwa huu huambukizwa kupitia vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex). Ugonjwa unaweza kujitokeza kwenye sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na kwenye puru (rectum).
Ugonjwa wa gono huonekana sana kwa vijana, watu wenye
maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi mijini, watu weusi na watumiaji madawa ya kulevya.
Dalili za ugonjwa wa kisonono
Dalili za ugonjwa wa kisonono huanza kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7 baada ya mtu kupata maambukizi na huweza kuchelewa kwa wanawake.
Dalili ni kama zifuatazo;
Kwa wanaume:
Kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa (burning sensation) Kutokwa na majimaji ya njano au meupe au ya kijani kutoka kwenye uume yanayoambatana na maumivu makali sana Wakati mwengine maumivu au kuvimba kwa korodani (swollen testicles) Maambukizi yakiwa kwenye puru (rectum) huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuwashwa sehemu za haja kubwa, na hata haja kubwa inaweza kutoka ikiambatana na damu, hii inatokea kwa wanaume na wanawake.
Dalili kwa wanawake huwa si nyingi lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili zozote Maumivu au kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa Kuongezeka kwa kutoka majimaji kutoka kwenye tupu ya mwanamke ambayo ni ya njano au yamechanganyika na damu Kutokwa na damu kupitia tupu ya mwanamke kabla ya hedhi kufika. Kutokwa na damu baada ya kujamiana au baada ya tendo la ndoa Kichefuchefu Homa (fever)
Kutapika
Vipimo vya ugonjwa wa kisonono’
Swab for culture – Kipimo hiki hufanyika maabara kwa kupandikiza bakteria baada ya kufuta sehemu za siri kwa kutumia swab ili kuona kama kuna bakteria wanaosababisha gono. Polymerase Chain Reaction (PCR) – Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya bakteria, ni ghali sana.
Tiba ya ugonjwa wa kisonono ni nini?
Tiba ya gono inahusisha na tiba ya ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi magonjwa haya huambatana kwa pamoja.Tiba hutegemea na umri wa mgonjwa na kama mtu ni mjamzito au la. Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra na puru, dawa zinazotumika ni aina za cephalosporin dozi moja pamoja na dawa za aina ya macrolide antibiotics (mfano azithromycin) na za jamii ya penicillin (mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa chlamydia.
Mara nyingi kwa wale chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano.