Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:22 pm

DKT BASHIRU: TULIHOFIA UMOJA WA KITAIFA WANACHAMA CUF KUHAMIA ACT WAZALENDO

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Bashiru Ally amesema kuwa mvurugano uliotokea ndani ya CUF na kufanya baadhi ya wanachama wake kuhamia chama cha ACT Wazalendo ni jambo lililoleta shida kwao, kwasababu ya kuhofia umoja wa kitaifa kuvurugika na kwamba CCM ipo tayari kufanya kazi na chama chochote. “Hata ile shusha tanga pandisha tanga haikuwa na shida ila tu isiathiri umoja wa Kitaifa na wala amani.

Dkt Bashiru ameyasema hayo leo Aprili 26 katika kipindi cha Gumzo la Muungano kilichorushwa live na Shirika la Utangazaji la Zanzibar (ZBC 2) chini ya Mtangazaji nguli nchini Tido Mhando.

Dkt Bashiru amesema hata wao walipingwa na mshangao kwa sababu hawakuwa kufikiria kuwa chama kama CUF kinaweza kuwa na mgogoro unaoweza kuwagawa kabaisa

"Maana hata sisi tulishtuka na hatukutarajia mabadiliko yale kwa sababu hatukuwahi chama kama kile kinaweza kuwa na mgogoro wa ndani unaoweza kusababisha mpasuko lakini tunamshukuru Mungu mambo yameenda salama.” “Lakini hatukushtuka kwamba kunaenda kutengenezwa chama kitakachoitikisa CCM hapana, kwa sababu sisi hatupati tishio kutoka vyama vya siasa ila tunapata tishio baada kuona mgogoro ndani ya chama kwa sababu tunataka kushindana na vyama madhubuti,” amesema Bashiru.

Pia Dkt Bashiru amesema kuwa ACT Wazalendo bado sio tishio kwao, hii ni mara baada ya kuulizwa swali na muongozaji wa mahojiano hayo, Tido Mhando. Dk Bashiru amesema chama hicho si tishio kwa CCM kwasababu kina na mwakilishi mmoja bungeni na kinaongoza halmashauri moja ya Kigoma Mjini, hivyo kuongezeka kwa wanachama huenda ikawa fursa kwao ya kuongeza wawakilishi.