- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
DKT. BASHIRU: CCM NI CHAMA CHA UONGOZI, SIO CHAMA CHA KUVUNA PESA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, amesema chama cha Mapinduzi CCM sio chama cha kuvuna pesa, misingi ya CCM ni kutoa uongozi, si kujilimbikizia pesa kama vinavyohubiri baadhi ya vyama vya siasa nchini.
Bashiru ameyaeleza hayo, Jana Jumapili Desemba 22, 2019 aliposimamishwa na mamia ya wananchi wa kata ya Kasharunga wilayani Muleba Mkoani Kagera akiwa njiani kuelekea Bukoba kwa mapumziko ya siku kumi
"Chama chetu ni chama kikubwa, kimeanzia ngazi ya shina, unapokuwa kiongozi au mwanachama ni heshima kubwa umepewa, sisi sio wavuna mapesa kupitia kwenye uongozi, kama wanavyojinadi wengine, sisi chama chetu ni chama cha uongozi pesa inakuja kwa kuchapa kazi sio kuihubiri." Dkt. Bashiru amesisitiza.
Ameeleza pia, umuhimu wa kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kutimiza malengo tuliojiwekea kuanzia ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.
Aidha, Dkt. Bashiru amefafanua baadhi ya malengo ya CCM katika kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja ikiwa ni pamoja na kuunganisha barabara zote kuanzia zile za mikoa, wilaya, kata hadi vijiji, upatikanaji wa mitandao ya simu, umeme, maji na huduma za afya kila kijiji.
Ambapo ameeleza kuwa, "CCM inataka maendeleo vijijini, vijiji viwe ni sehemu za uzalishaji mali na viwe ndio vitovu vya maendeleo yetu". Katibu Mkuu amesisitiza
Mapokezi hayo, yameongozwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Muleba Ndg. Athumani Kahara na Mkuu wa wilaya hiyo Ndg. Richard Ruyango.