Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:57 pm

DIAMOND PLATNUMZ "SITAKI MWANANGU TIFFAH AFANYE MUZIKI WATAMLA SANA"

Nairobi: Msanii wa muziki wa bongo fleva Naseibu Abduli A.K.A Diamond Platnumz amesema kuwa hayuko tayari kumruhusu Mwanae wa kike Tiffah kufanya muziki, Diamond alieleza hayo wakati akihojiwa kwenye kipindi cha The trend kinachorushwa na kituo cha televisheni cha NTV cha nchini kenya,

Diamond aliulizwa kuwa kama angependa wanae kuwa wasanii au wafanye shunghuli nhyingine, "Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii kwa sasabu watamla sana" alisema kuwa mwanamke kama mwanamke nikweli anaweza kutongozwa lakini anapokuwa msanii watu wanao mjua wanakua wengi na watu wanao kujua wanapokuwa wengi kutongonzwa kunakuwa kwingi wataniua na presha" aliongea Diamond

Hit singer huyo pia alitumia nafasi kidogo kuongelea msiba wa IVAN ambae alikuwa baba watoto wa mpenzi wake wa sasa ZARI baada ya mtangazaji kumuuliza swali la kuhusu msiba huo.

Mtangazaji alihoji kuwa watu wanasema Zari amemtembelea baba watoto wake hospitalini wakajua kuwa Diamond hatakuwepo "kiukeli ilikuwa wakati mgumu mpaka sasa hivii umekuwa wakati mgumu kwa sababu nilikuwa niko booked namsiba ndo umetokea sasa kui cancel show yawatu inawezekana ukapata taswira tofauti wengine wakachukulia tofauti lakini niliongea na mzazi mwenzangu akanielewa" aliongea Diamond