- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
CHADEMA: SPIKA NDUGAI 'AMELIPOTOSHA BUNGE' KUHUSU MALIPO YA LISSU MIL 270
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimekanusha vikali taarifa ya spika wa Bunge la Jamhuri ya muungano, Job Ndugai, kuhusu taarifa ya matibabu ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Ndugai amesema kuwa kama bunge limesha mpatia mbunge huyo kiasi cha Shilingi milioni 270 kama pesa ya Mataibabu.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho kwa vyombo vya habari jioni ya leo, tarehe 31 Januari 2019, imemuita spika huyo kuwa “muongo na mbobezi wa upotoshaji."
“Spika wa Bunge, Job Ndugai amelipotosha Bunge na ameudanganya ulimwengu kuhusu matibabu ya mbunge wetu, Tundu Lissu. Spika wa Bunge, ni kiongozi wa umma. Hivyo ni fedheha kiongozi wa umma kuwa muongo,” imeeleza taarifa hiyo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kipindi cha maswali na majibu, bungeni mjini Dodoma, Spika Ndugai alisema, Bunge limetoa takribani Sh. 270 milioni, kwa ajili ya kuhudumia matibabu ya mwanasiasa huyo.
Kwa takribani mwaka mmoja na nusu sasa, Lissu amekuwa kwenye matibabu yanayotokana na shambulio la lisasi za moto lilitokea nyumbani kwake, Area D, mjini Dodoma.
Katika taarifa ya Chadema inasema, Lissu hajatibiwa na Bunge wala serikali. Bali, ametibiwa na chama chake, michango kutoka kwa wananchi na wanachama wa wengine wa chama hicho, wabunge na madiwani.
“Lissu ametibiwa na chama chake, wanachama mmoja mmoja, mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi, Watanzania washio ndani na nje ya nchi na wabunge waliochanga kiasi cha Sh. 43 milioni,” imeeleza taarifa hiyo.
Chadema kinasema, kimelazimika kumjibu Spika Ndugai kwa kuwa bila haya na kwa makusudi ameamua kuliongopea bunge na kuungopea ulimwengu.
“Alichopewa Lissu ni stahiki zake za lazima; na siyo pesa ya matibabu kama alivyoeleza Spika Ndugai. Ni uwongo wa mchana kusema kuwa Lissu amepewa kiasi cha Sh. 270, wakati hicho alichokipata, ni stahiki zake.”
Aidha, taarifa hiyo inasema, “…spika amedai yeye anazo nyaraka za uthibitisho wa malipo ya matibabu ya Lissu. Tunamtaka atoe hizo nyaraka hadharani na siyo kutishia ili kuhalalisha uongo wake.”
Naye Lissu anasema, Bunge la Jamhuri ya Muungano, halijawahi kutoa hata senti tano kugharamia matibabu yake.
Lissu ametoa kauli hiyo, muda mfupi baada ya Spika Ndugai kusema, Bunge limetoa kiasi cha Sh. 270 milioni kulipia matibabu yake.
Amekiri kulipwa Sh. 43 milioni zilizotolewa na wabunge wenzake kama mchango wao kwa matibabu yake. Anasema, kiasi cha fedha kinachotajwa – Sh. 250 milioni – ni mishahara na stahiki zake nyingine, na siyo gharama za matibabu.