Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 11:39 am

CAG PROF MUSSA ASSAD: NINAKWENDA KULIMA BAMIA BAAADA YA HAPA

Alikuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Profesa Mussa Assad amesema kuwa anakwenda kufanya kilimo kutokana na uwekezaji alioufanya katika siku za hivi karibuni baada ya kustaafu nafasi hiyo, akinadi kwamba watu mjini wakimuhitaji atarudi kuja kusaidia .

Profesa Assad ameyasema hayo Leo Jumanne November 5, 2019 wakati wa makabidhiano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT),leo jijini Dar es Salaam.

Profesa amesema kuwa katika kufanya kazi amewashukuru wafanyakazi wa ofisi hiyo kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha utumishi na kumtaka CAG mpya afanye ushirikiano nao kwani watu hao wamejengwa kwa muda mrefu na sifa zote .

Assad amesema kuwa katika kufanya kazi tumejenga mahusiano na wadau mbalimbali wa nje ambao ndio watu wa kujengeana uwezo na sio kwa ndani

“Changamoto ni nyingi tumepitia lakini siwezi kutia ukakasi katika hili na watu niliowakosea, naomba wanisamehe kwani sisi ni binadamu”amesema Profesa Assad

Kwa upande wa CAG Charles Kichere mpya amesema kuwa kazi kubwa ni kulinda kihenge anajua kazi ngumu ya ukusanyaji wa mapato.

Kichere amesema ataifanya kazi hiyo kwa weledi na uadilifu kwa kushirikiana na timu yake ya ofisi ya Taifa ya mkaguzi ikiwa na kuangalia mapato ya nchi yanatumikaje kwa kuangalia ripoti sambamba na kujenga timu imara na sio watu walisambaratika.