Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 7:42 pm

BURUDANI : WAKATI DIAMOND AKIKUBALI MTOTO,ZARI ACHEFUKA

Msanii Diamond Platnumz amekubali kuwa mtoto wa hamisa mobetto ni mali yake

-Adai alituma milioni 7 za kumpeleka hamisa hospitali

-Kila wiki hamisa aingiziwa laki 5 za matumizi

-Jina la Abdul hajui limetokea wapi

Msanii wa Kizazi kipya Naseeb Abdul,Diamond Platnumz ameibuka na kumaliza migongano juu ya nani baba wa mtoto Abdul aliyejifungua Mwanamitindo na Video Queen Hamisa Mobetto siku kadhaa zilizopita

Kupitia Instagram akaunti ya mtoto Abdul, hamisa aliweka wazi kuwa mtoto huyo ni mali ya msanii Diamond Platnumz hivyo kukiuka ahadi walizoeka juu ya namna ya kumtambulisha mtoto huyo

Msanii Diamond amekubali kuwa mtoto aliyezaa na Hamisa Mobetto ni wake na hakumkataa mtoto huyo kama ilivyodaiwa awali katika baadhi ya mitandao ya kijamii,pia Diamond ameoneshwa kukasirishwa kufuatiwa Mlimbwende Hamisa kuweka baadhi ya picha zikionesha kuwa na Diamond katika baadhi ya maeneo yanayoashiria kuwa mtoto huyo ni mali ya msanii huyo

akiendelea kufunguka msanii huyo amedai waliweka ahadi kati yake na hamisa juu ya kutomtambulisha mtoto huyo kwa muda huu mpaka pale muda utakapofika,lakini chakushangaza mzazi mwenzake Hamisa ndiye aliyekiuka ahadi hiyo na kuanza kumtaja mapema kwenye mitandao kuwa Diamond ndo baba wa mtoto wake

kufuatiwa baadhi ya wadau kusema Diamond alimkataa mtoto,amekanusha shutuma hizo na kusema sio kweli na haijawahi kutokea,na mara zote amekuwa akimtumia hamisa pesa za kulea ujauzito mpaka kujifungua

"Hamisa alipata ujauzito wangu kweli alinieleza nikamuambia kama baba mwenye familia yangu naomba ulinde heshima yangu na hata hivyo Mtoto kabla ya kuzaliwa nilitoa shilingi mil. 7 na nikampeleka hospital ya Private kwa ajili ya kujifungua"alisema Diamond


baada ya kufunguka mengi pia nyota huyo wa muziki alisema kwa upande wa mzazi mwenzie anayeishi nchini Afrika ya kusini,Zarina Hassan alimueleza suala hilo kwa ufanisi na hakuwa na shida kwani alikubaliana na hali halisi lakini tatizo lilikuwa kwa Hamisa ambaye mara zote alikuwa na kawaida ya kuweka picha mitandaoni kwa lengo la kumkoa msanii Diamond Platnumz

"Zari aliniuliza kuhusu mimba ya hamisa nikamwambia ukweli na akanielewa, Zari hana noma na yule mtoto, anajua kila kitu"alisema Diamond

Inaonekana kama Zari The Bossy alikuwa akiskiliza Diamond alivyokuwa anaongea maana kauli hii pia ilionesha kumchefua mrembo huyo na kuonekana kama ni uongo aliotumia Msanii Diamond baada ya muda mchache kuposti Instagram na kuandika

Tafsiri:ameanza kwa kucheka kidogo ! Haha unajichezea mwenyewe....uongo unaosema kuhusu mimi,kuhusu upande wako...kujaribu kutatua madudu yako,na acha kusema uongo.mimi kua kimya haimanishi ni mpumbavu.kuwa makini na maneno yako-ameandika zari The Bossy Lady


Anaendelea tena: Tafsiri:Ni kwa sababu mimi ni mama wa watoto wako ndio maana nakaa kimya & na kuweka heshima unaweza kutaka nikufungulie kesi ya kashfa ya maneno ya uongo"usinijaribu !!!! alimaliza Zari the bossy lady

Kwasasa msanii Diamond ni baba wa watoto wanne ,ambao amewapata kupitia mama tofauti,tayari amezaa na mrembo zarina watoto wawili,na mwingine ni msichana aliyezaa naye mwanza,na wamwisho ni Hamisa Mobetto ambaye amezaa nae hivi karibuni na mtoto huyo kupewa jina la Abdul,ambalo ni jina la baba mzazi wa Diamond Platnumz.