- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI: SHILOLE: 'SIWAHITAJI WANAUME WENYE PESA'
Msanii wa bongo Flava Zuwena Mohamed maarufu kwa jina la ' Shilole' anayetamba na hit ya 'hatutoi kiki' amefunguka na kudai kwamba haitaji kuolewa na mwanaume mwenye pesa kwani wengi wao hutumia mali zao kama fimbo ya kuwachapa na kunyanyasia wanawake zao.
Ameyasema hayo katika ukurasa wa Facebook wa EATV, Shilole amefunguka kuwa yupo tayari kuolewa lakini mpaka atakapo pata mwanaume atakayekidhi vigezo vyake huku akitaja pesa siyo kitu anachokitanguliza bali heshima, upole na ukarimu.
"Natamani sana kuolewa lakini mpaka nimpate mtu mwenye vigezo ninavyohitaji mimi, napenda mwanaume anayejali, atakayeniheshimu lakini awe pia anafanya kazi kama hafanyi kazi simtaki. Lakini pia wanaume wenye pesa siwataki maana tunawaona huko majumbani wanavyotumia kama fimbo kuwanyanyasa wake zao" Shilole alifunguka.
"Mimi siangalii sana muonekano kwani unaweza kutengenezwa lakini ukiwa mfupi mimi sitakukubali nahitaji mwanaume mrefu na mwenye heshima na anayejituma kwenye utafutaji" aliongeza Shilole.