- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
Burudani: nyimbo za bongo fleva zaongoza kwa kutazamwa zaidi kwenye YouTube nchini Kenya
Nairobi: ripotI iliyo tolewa jana na wawakishi wa mtandao maarufu wa video Duniani YouTube unaripoti kuwa katika chatI ya video kumi zinazotazamwa Zaidi nchini Kenya ngoma 3 zinatoka nchini Tanzania
Video hizo zinatawala katika orodha ya video kumi zilizotazamwa zaidi, inayoongoza ikiwa video ya wimbo Salome, uliofanywa upya na Diamond Platnumz na Rayvanny.
Wimbo wa Work, wao Rihanna na Drake ni wa pili lakini kutoka hapo anaingia Diamond Platnumz na Harmonize wakiwa na wimbo wao bado
Video ya kwanza ya Wakenya kwenye orodha hiyo ni ya Sauti Sol kwa wimbo wao Unconditionally Bae, lakini bado kwenye wimbo huo walishirikiana na mwanamuziki Mtanzania, Alikiba.
Video nyingine za nyimbo katika orodha hiyo ni Work from Home wa Mmarekani Ty Dolla Sign na kundi la wasichana la Fifth Harmony, This is What You Came For wake raia wa Scotland Calvin Harris, Kwetu wake Rayvanny kutoka Tanzania, Cheap Thrills wao raia wa Australia Sia na Sean Paul wa Jamaica, Pillow Talk wa Mwingereza Zayn na Ain't Your Mama wa Mmarekani Jenniffer Lopez.
Orodha tazama hapa:
- Salome - Diamond Platnumz na Rayvanny
- Work - Rihanna na Drake
- Bado - Harmonize na Diamond Platnumz
- Sauti Sol - Unconditionally Bae, na Alikiba.
- Work from Home - Ty Dolla Sign na Fifth Harmony
- This is What You Came For - Calvin Harris
- Kwetu - Rayvanny
- Cheap Thrills - Sia na Sean Paul
- Pillow Talk - Zayn
- Ain't Your Mama - Jenniffer Lopez.