- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BURUDANI: FAIZA ALI AONESHA MAPENZI YAKE KWA DIAMOND PLATNUMZ
Dar es salaam: Muigizaji na Mwanamitindo mashuhuri Tanzania Faiza Ally amesema kuwa haoni haja kwa watanzania kutokumpendi na kujivunia kwa Msanii Diamond Platnumz kwa sababu yeye ndio kafanya muziki wa Tanzania kuwa wa International na kuwa muziki wa Kiushindani hapa Bongo "Hivi mnajua kwamba Tanzania nzima na East Africa tunatakiwa tumpenda Diamond sana ???? Hivi hamjawaji kujiuliza kwamba toka zamani kabla ya Diamond kulikua na mziki mzuri lkn hakujawahi kuwa na ushindani kama changamoto alio leta Diamond kwenye game , sasa nasema hivi mziki mzuri peke yake hautoshi na akili kubwa inahusika , unapo kuwa huna akili ktk unalo lifanya ni sawa na mwanamke mzuri hlf hajielewi"
Akiandika kwenye Ukurasa wake wa instagram Faiz amesema kuwa uwepo wa mafanikio ya Diamond Platnumz umefanya mpaka wazazi wa leo wanahitaji watoto wao kufanya muziki, kwa sababu unamafanikio sana.
"Leo hii kwa u star wenye akili alio uleta Naseeb wazazi wengi wanaona fursa ya mziki kupitia Diamond tofauti na miaka ya zamani, mziki ulikua unaonekana kama sio kazi lkn Leo mziki unaendesha familia nyingi, hata mm ningependa mwanangu awe mwanamziki mwenye mafanikio kama Diamond "
"sasa nasema hivi ku mpenda Diamond ni amri sio ombi, Diamond ni kama Obama marekani kwa watu weusi , yeye alionyesha kuwa mtu mweusi ana uwezo kwenye siasa na Diamond tanzania kaonyesha mziki unalipa na msisahau katoa vijana wengi na bado wengine wamepata ajira kupitia yeye na naona watapata wengi zaidi ! Sasa nakuomba D ufungue music school basi tuwalete watoto wetu na wenyewe wapate mkwanja kama wako maana shule sio maisha pekee mention town na vipaji navyo ni sehemu ya mafanikio ktk maisha a special kwa maisha tunayo elekea , mm nakupendaga sana na zaidi ni jitihada zako kwenye kazi ! Keep it up dogo" alimalizia faiza