Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 6:42 pm

BURUDANI: DIAMOND AWAJIBU MBOVU HATES JUU YA MPENZI WAKE ZARI

Dar es salaam: Mwanamuziki maarufu Africa mashriki Naseib Abdul A.K.A Diamond Platnumz jana aliamua kuwavulia uvivu watu wanao msema Baby mama wake Zari Hassani kuwa badala ya kuomboleza msiba wa mama yeake ambaye alifariki mnamo tarehe 15 july mwaka huu yeye anaponda raha na Diamond,

"Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa Misiba ya watu.... Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehem tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja!...sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo,

Diamond alisema kuwa mfumo wa kila anaye fiwa si lazima ajifungie chumbani kulia, kwani huwa si utamaduni wa kila mtu.

" Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia... Pambaneni na Mahusiano yenu...!

Diamond alimalizia kwa kusema kuwa yupo kwenye kumfariji mama watoto wake kwa muda wa siku 5 na kusema kuwa siku ya jana ndio ilikuwa ya kwanza

"Nina siku 5 za kumpetipeti... leo ndio kwanza Ya kwanza "