Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 9:33 pm

BURUDANI: BEN POUL:'' KWANI KIPATO KIKUBWA KINATOKANA NA DILI ZA HAPA NYUMBANI ''

DAR ES SALAAM: Msanii Ben Poul amejibu tuhuma zilizotolewa na kampuni ya kimataifa ambayo ilimsajili kusimamia kazi zake ya Pana Music, kwamba wasanii wengi wa Tanzania wanafeli kwenda kimataifa kwa sababu muziki wao unalenga soko la ndani pekee.


Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television Ben Pol amesema msanii yoyote hapa nyumbani soko la ndani ndio muhimu, kwani kipato kikubwa kinatokana na dili za hapa hapa ndani, tofauti na zile za nje.

"Tukubali tukatae, mpaka sasa hivi tunavyozungumza 'potential market' ya muziki wetu ni Tanzania, vipato vya wasanii na maproducer asilimia zaidi ya 85 vinatokea nyumbani, kwa hiyo hapa tukiongelea mifano ya wasanii wenzetu ambao wana kasi zaidi ya kimataifa, tukiangalia soko lao, source za vipato vyao kwa asilimia kubwa wanavipata kwa Watanzania wenzao na kwa makampuni ya Tanzania, hii inamaanisha kwamba soko la nje kasi yake ni ndogo kidogo", alisema Ben Pol.

Pia Ben Pol amesema kitendo cha mtu kukwambia uache soko la muziki la ndani na kufikiria la nje sio kitu kizuri, kwani soko la nje kwa wasanii wa Tanzania bado halijafanikiwa kwa asilimia kubwa.

"Hatutakiwi kukata tamaa, hatutakiwi kuishia njiani, mtu akikwambia uachane na soko la ndani huyo ni adui yako, lazima ulinde soko lako la ndani alafu hayo mengine ndiyo yanaongeza soko la nje", alisema Ben Pol.