- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BUNGE LAITAKA IKULU YA MAREKANI KUTOA NYARA ZA MAWASILIANO ZA UKRAINE
Kamati za Bunge la Marekani zinazoendesha uchunguzi dhidi ya rais Donald Trump zimeiamuru Ikulu ya White House kuwasilisha nyaraka zote za mawasiliano kati ya Trump na Ukraine.
Amri hiyo imetolewa baada ya Ikulu ya Marekani kushindwa kuchapisha kwa hiyari nyaraka hizo kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho jana Ijumaa. Moja ya viongozi wa kamati za Bunge la Marekani amesema ni wazi rais Trump amechagua njia ya kuficha ukweli baada ya kushindwa kwa mwezi mzima kuweka wazi nyaraka za mawasiliano yake na Ukraine.
Hapo jana, rais Trump alisema huenda asitoe ushirikiano kwenye uchunguzi dhidi yake ambao unahusu madai kwamba alimshinikiza rais wa Ukraine kumchunguza makamu wa rais wa zamani Joe Biden na mwanawe kwa tuhuma rushwa.