Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 11:38 pm

BUGE NEWS: "ZIFAHAM SABABU ZA VITU KUPANDA BEI NCHINI" WAZIRI MPANGO ANAELEZA

Dar es salaam: Waziri wa fedha na mipango Dr. Philipo mpango leo amefafanua sababu ya kupanda kwa mfumuko wa Bei hapa nchini ambapo alitaja sababu kama Uwepo wa ukame katika maeneo ya ukanda wa Afrika mashariki, sababu ya pili mwenendo wa kushuka kwa bei ya petroli kwenye soko la Dunia na nchini, sababu nyingine kuimarika kwa upatikanaji wa chakula nchini, kuwepo kwa sera madhubuti za usimamizi wa bajeti na fedha na Hofu kwa kuchelewa kwa msimu wa mvua katika maeneo mengi nchini. aliyasema hayo leo mjini Dodoma kwenye mkutano wa 7 wa bunge la Jamhuri na kuwasilisha mpango wa serekali kwa mwaka 2017/2018

Mpango pia alisem kuwa mfumko wa bei Duniani umeongezeka kwa wastani wa asilimia 2.9% kwa mwaka 2016 ambapo ni zaidi ukilinganisha 2.8% kwa mwaka 2015. Mfumko wa bei nchini ulipungua kutoka asilimia 5.6% kwa mwaka 2015 mpaka 5.2% kwa mwaka 2016. alisema kuwa kwa mwezi 5 mfumko wa bei ulishuka mapak asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.4% kwa mwezi wa nne.

Hata hiyo Dr. Mpango alisema kuwa pato la Taifa limekuwa kwa asilimia 7% kwa mwaka 2016 ambapo ni shini ya malengo ya kufikia asilimia 7.2%, akasema kuwa wastani wa pata la taifa kwa kila mmoja kwa mwaka 2016 ni Tsh milioni 103,744,660/= ambapo ukiligawa kwa idadi ya watu kitaifa ambapo inakadiriwa kuwa na watu milioni 48.6 hii itakuwa ni sawa na kila mmoja kuwa na Tsh milioni 2,131,299 ambapo kwa kiwango hichi cha mwaka 2016 ni zaidi ukilinganisha kwa mwaka 2015 ambopo pata la mtu moja moja lilikuwa ni milioni 1.9.