- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
BOBI WINE " MASHTAKA MENGI YA KIPUMBAVU YANAENDELEA DHIDI YETU"
Serekali nchini Uganda imemfungulia mashtaka katika mahakama kuu Nchini Humo mbunge wa upinzani na mwanamuzi Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine na watu wengine zaidi ya 20 kwa kumkasirisha rais Yoweri Museveni.
Mbunge huyo aliyetangaza nia ya kuwania urais mwaka 2021, aliongezewa shtaka hilo, baada ya kuanza kwa kesi hiyo Jumanne wiki hii jijini Kampala, kutokana na mashatka mengine yanayomkabili ya kurushia mawe msafara wa rais Museveni mwaka uliopita.
“Mashtaka mengi ya kipumbavu yanaendelea kuwasilishwa dhidi yetu, napenda kuiambia dunia kuwa, hii haitutishi kwa njia yoyote ile”, amesema Bobi Wine.
Wine nakabiliwa na kifungo cha maisha jela, iwapo atapatikana na hatia.
Wine ambaye jina lake ni Robert Kyagulani bado anakabiliwa na mashtaka katika mahakama nyengine kwa kuongoza maandamano dhidi ya sheria inayoweka kodi katika mitandao ya kijamii pamoja na biashara zinazofanywa kupitia malipo ya simu za rununu 2018.
Msanii huyo ambaye amekuwa mwanasiasa wa upinzani anayepinga utawala wa miongo mitatau ya rais Museveni hivi majuzi alitangaza kwamba atawania urais katika uchaguzi wa 2021.