- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
ASKARI WAUA WASHUKIWA WATATU SHAMBULIO LA KIGAIDI JIJINI LONDON JUMAMOSI JIONI
LONDON:Watu saba wameuwawa na wengiune wasiopungua ishirini wamejeruhiwa katika shambulio linalotajwa kuwa ni la kigaidi kwenye daraja la London, uingereza.
Washambuliaji walianza na kuwagonga waenda kwa miguu wakitumia gari kubwa la kusambazia mizigo kwa maksudi na kasi, kisha watu hao walishuka na kuanza kuwashambulia watu waliokuwa eneo hilo kuelekea soko la Borough kwa kuwachoma visu, watu wengi walijeruhiwa huku taarifa za dharula zikwafikia polisi ambao waliwadhibiti kwa kiasi wahalifu hao, askari waliwaua washambuliaji watatu,na raia watat walikwishauawa na waharifu hao na kufanya idadi kufikia sita. Mashuhuda wa tukio hilo wanadai kuwa magaidi wawili walifankikiwa kutoroka eneo hilo.Polisi wamethibitisha mapema leo hii kuhusu taarifa hizi na kutangaza kuwa ni tukio la kigaidi na kwamba majeruhi wamepelekwa katika hospitali mbalimbali za jijini hapo,wameongeza pia washambuliaji hao walivaa mabomu ya kujilipua nayo ambayo ni feki. Ikumbukwe kwamba ni siku chache zimepita kutoka shambulio la kujitoa muhanga lifanyike nchini humo katika mji wa Manchester na kupoteza maisha ya watu takribani 22 na majeruhi wengine. Mataifa makubwa duniani, Marekani na Ufaransa, kupitia maraisi wao wamesema wapo tayari kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na ugaidi, raisi Donald Trump na Emmanuel Macron.
Kwa upande wa Ujerumani tamasha kubwa la muziki lijulikanalo kama Rock au βRock am Ringβ imeripotiwa kuwa litafanyika bila tatizo lolote kwani waandalizi wa tamasha hilo wamedai matukio hayo ya kigaidi hayana msingi kwao wala hayaleti hofu kiusalama uelekea tukio hilo kubwa.