Home | Terms & Conditions | Help

May 18, 2024, 2:40 pm

SPORTS: FAHAMU UBUNIFU WA JEZI YA YANGA KWA MSIMU 2022/2023

Dar es salaam. Club ya Wanajangwani ya Yanga usiku wa kumakia leo Julai 29 imetambilisha jezi yake mpya kwa msimu wa 2022/2023. Jezi hizo zimebuniwa na Mbunifu mkongowe wa mavazi wa muda mrefu Sheria Ngowi na sasa Jezi hizo zitasambazwa na kuuzwa na wadhamini wao GSM company.

Katika jezi hizo yanga imefanya ubunifu mkubwa sana, Ubunifu wa jezi ya nyumbani (home kit) ya Yanga imeanzia kwenye kutangaza maeneo yote muhimu na ya kihistoria kwenye nchi ya Tanzania kama Mlima Kilimanjaro, Nyerere Square Dodoma, Ngome Kongwe Zanzibar, Jengo la Yanga pale msimbazi na vingine vingi.

Jezi ya Ugenini ya Yanga kwa msimu wa 2022/2023.

Jezi ya ugenini ya Yanga inaelezea muunganiko wa Matawi ya wanachama wa Yanga Tanzania nzima ikichagizwa na mfumo wa mabadiliko (transmission)

Jezi ya Yanga ya Tatu (third kit) msimu wa 2022/23

Hadithi ya jezi ya Tatu inawahusisha Wachezaji wa Yanga wa zamani (legends) kwa kufanya makubwa katika sehemu ya historia ya Klabu yetu na jezi hii imebuniwa kwa kuwaandika majina yao kwa mfumo wa sahihi (signature)